SWAHILI Radio Script - The Media
REACH FOR LIFE PROGRAM
KIPINDI: AFIKIO LA KUISHI
Swahili Translator: Kaindo Stefano
Live 1 – The Media
Hujambo na karibu. Hiki ni kipindi cha Afikio la Kuishi..
Host 1: Jina langu ni Kaindo Stefano, nami nina afikio la kuishi.
Host 2: nami ni Wambui ngari na vilevile nina afikio la kuishi.
*Host 1: kumbuka, Afikio la kuishi ni uamuzi wako binafsi!
Host 2: kwenye kipindi cha leo, mie na mwenzangu Stefano tutakueleza ni kwa sababu gani tuna afikia kuishi na wakati uo huo nikueleze kuhusu kipindi hiki kipya cha Afikio la Kuishi.
*Music – Maisha ya Mwanadamu (Mary Atieno)
Host 1: Ni wimbo wenye baraka na unaotoa mwongozo wa maisha. Wimbo wake Mary Atieno. Hii ndio aina ya burudani unayoipata hapa. Kipindi ni afikio la kuishi, kipindi kinachofanikishwa na Biblica kwa ushirikiano na TransWorld Radio Kenya. Jina langu ni ….Kaindo Stefano naye mwenzangu hapa binti mwenye sauti nyororo ya kumtoa nyoka pangoni akiwa ni Wambui Ngari……
Host 2: Mwenzangu stefano, kuna dhana eti kuwa kijana mdogo kuna ugumu wake. Pia maswali kuhusu ujana ni mengi huku majibu yakionekana kuwa machache. Na wakati mwingine, hata viongozi wa makanisa, wazazi, na pia marafiki zetu hukosa kutuelewa sisi vijana.
*Host 2: na ndio maana (drum roll…) Afikio la Kuishi limezinduliwa. Tutatembea Pamoja kwenye swala hili ambalo lina mwongozo wa Bibilia. Ikiwa ni Amini, Komaa, ishi, na kubadilika. Kwa hivyo Stefano Kuanzia leo…
Host 1: … Samahani wambui, kuanzia sasa hivi!
*(kicheko) naam kuanzia sasa hivi tunaanza na Livejourney yaani safari ya Kuishi.
*Host 1: The live journey safari ya kuishi inatuelekeza jinsi ya kukabiliana kikweli na changamoto za maisha haswa kwa sisi vijana.
Je, unataka kuishi maisha marefu? Basi endelea kuwa nasi. Leo tutajifunza kuhusu vyombo vya habari. Ni kwa njia gani kile tunachosoma, kutazama na pia kusikiliza kinavyoathiri maadili yetu na safari yetu na Mungu? Hebu tusikilize…
Instrumental
Title: Vyura wanaochemshwa!
SIKILIZA
Voice: inasemekana kwamba, chura aliye katika chungu cha maji yanayochemka taratibu, hawezi kuruka, kwa sababu hatambui mabadiliko ya taratibu ya ongezeko la joto. Vyombo vya habari ( muziki, sinema, magazeti, runinga, redio na mitandao) zinaweza kuua taratibu maadili ya kiungu na mwenendo wetu na Mungu, pasipo sisi wenyewe kugundua. Vyombo vya habari vinasambaza uongo ambao kama hatutakuwa makini nao, utaua wetu na imani. Huu ni uongo kama: Fanya ngono ovyo!’ “ni sahihi kulipiza kisasi” “Kuwa Tahiti, mrembo na maarufu vitakupa furaha!” “Dini zote zinatuongoza kwa Mungu!” “ Usimruhusu mtu yeyote kujueleza namna ya kuishi-ni maisha yako!” na “Mungu na imani ni vitu vilivyopitwa na wakati!”
Instrumental
Tujifunze “kuruka” kutoka uongo na kukwepa mioyo yetu isipikwe taratibu wakati huo!
Host 1: habari ndio hiyo wambui… ni vyema “kuruka” na kujiepusha na uongo ambao vyombo vya habari vinatupasha ili kuzuia kupikwa kupitia uongo. Maelezo hayo ni ya mfano na ya kupendeza.
*asante sana Njeri Thuku - unasikiliza kipindi cha Afikio la Kuishi kinacholetwa kwako na Transworld radio kwa ushirikiano na Biblica.
Host 2: bilashaka Stefano, kwa kweli, wakati mwingine taarifa tunazopokea zinauwezo wa kututenga na ukweli. Je, Bibilia inasema nini kuhusu hili? Hebu tuangazie na tujifunze na Bibilia. *Ila kabla Njeri Thuku atuelekeze kwenye somo la Bibilia, hebu tupate burudani ya muziki kwanza.
Music - Gloria muliro
*LOOK Robert (Tazama Njeri Thuku )
*Romans 12:1-2
Kwa hiyo ndugu zangu nawasihi kwa sababu ya huruma zake Mungu, jitoeni kwake muwe sadaka hai, takatifu na inayompendeza Mungu, ambayo ndio ibada yenu ya kiroho.2 Msiige tabia na mien endo ya dunia hii bali mbadilishwe, nia zenu zikifanywa kuwa mpya, ili mpate kuwa na hakika ni nini mapenzi ya Mungu: yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na makamilifu.
Romans 12:1-2
Instrumental bridge
JIFUNZE
Mungu ni mtakatifu na wa rehema(ms1). Uhusiano wetu naye unaanza kutubadilisha ili tuuonyeshe utakatifu wake kwa ulimwengu. Ni lazima tutoe kila eneo la maisha yetu kwa mungu kama kitendo cha ibada (Ms1).
……..
*Mungu wetu ni mtakatifu. lakini sisi tuna upungufu wa njia ya maisha anayotarajia kutoka kwetu. Ila tunamshukuru Mungu kwani ametuonyesha rehema zake. Rehema yake ya kwanza ni kuwa amemtuma Yesu ili afe kwa ajili yetu ili atupatanishe na Mungu. Rehema ya pili ni kuwa, amemtuma roho mtakatifu kuishi ndani yetu na kutufanya wapya ndani na nje. Rehema yake ya tatu ni kuwa ametupatia Bibilia ili kutupa ufahamu wa Yeye ni nani na jinsi ya kuishi.
Tunafaa kujibu vipi kuhusu Rehema hizi za kupendeza?
1. Mwabudu Mungu kwa nafsi yako yote. Kwa kumpa Mungu nafsi zetu na maisha yetu yote, uhusiano wetu na Mungu huanza kutubadilisha, ili tuige wema na ukarimu wake kwenye dunia.
2.“usiishi jinsi ulimwengu huu uishivyo”(v2). Tunazingirwa na utamaduni pale neno la Mungu na njia zake hazijulikani, haziheshimiki au kutiika. Popote tunapotazama, binadamu huonekana kana kwamba wanaishi kwa furaha na kutenda dhambi bila hata kumfikiria Mungu. Maisha hayo hutupa sisi changamoto ya kuwa kama wao, badala ya kubadilika na kuwa kama Yesu.
Tunaweza vipi kujiepusha na hili?
3. “ruhusu kubadilika kwa jinsi unavyofikiri (v2). Tunapobadilisha fikra zetu, tunabadilisha jinsi tunavyoishi. Kuishi uungu kunaanza na fikra za kiungu. Ndio maana tunastahili kulisha akili zetu na vitu bora. Fanya hivi kwa kujaza akili zako na neno la Mungu kila siku. Chochote unachosikia au kutazama, kiwianishe na neno la Mungu. Pia, chukua jukumu la kubaini unachotazama, unachosoma, unachofikiria na unachosikiliza. Kwa mfano, kutazama kanda za ngono na zile za vita, hakuchangii upya wa akili zetu.
Zawadi ya haya yote ni nini? Yakiwa ni kumwabudu Mungu kwa ukamilifu wetu? Kwa kukosa kuishi jinsi ulimwengu uishivyo? Na kwa kubadilisha jinsi tunavyofikiria?
Jibu ni: “Basi utaweza kujaribu ni nini haswa Mungu anapanga kwa ajili kwako. Na utakubali kuwa, anachopanga ni sahihi. Mipango yake ni miema, yakupendeza na kamilifu (v3).
Furaha iliyoje kuishi maisha ambayo Mungu anatutaka sisi kuishi!
LIVE
Host 1: Swadakta! Asante sana Njeri Thuku kwa neno hilo.
Hebu sasa tuusikilize wimbo wake Christina shusho - unikumbuke.
Wimbo – unikumbuke - Christina shusho
Host 2 Ni wimbo uliojaa ufasaha. Wimbo wake …Christina shusho.
Kipindi ni Afikio la Kuishi na leo tuko kwenye Safari ya Kuishi, tukijifunza kuhusu vyombo vya habari, na jinsi jumbe tunazosikia, kusoma, na kutazama, zinavyodhuru maadili yetu. Kama una swali lolote au himizo, na ungetaka kusema nasi, tutumie ujumbe mfupi au ukipenda SMS kwa nambari -.
Host 1: Ni namba ya simu inayokupa nafasi ya kutoa mchango wako, ikiwa ni -. Wambui, fikiria kuwa kila mmoja wetu ni simu ya mkononi - kumaanisha sio jumbe zote hutufikia. Basi tuna urahisi wa kuziamini jumbe na tamaduni ambazo hii dunia inatutumia.
Host 2: Hiyo ni picha nzuri sana. Sisi ni simu za kisasa yaani smartphones. Na mfano huo nimeuelewa vizuri kwani ni lazima tufuate watu wafaao na pia jumbe zifaazo. Na wakati zinatufikia, tunafaa kubaini ni jumbe gani zisizofaa.
Host 1: Kweli, tunafaa kufikiria vyema kuhusu wazo lolote. Kuna aya kwenye Bibilia ambayo hutueleza kuhusu aina ya vitu tunavyostahili kufikiria-na aina ya video, vipindi na sinema tunazofaa kutazama. Ndio hii hapa:
“Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima”.
(Philippians 4:8)
Host 2: Hilo ni neno nzuri sana. Ni kweli tunafaa kujua ni nini cha kutazama na ni watu gani tunaowasiliana nao kwenye mitandao ya kijamii.
Tunaweza kujiuliza maswali kama:
Je, jambo hili ni la kweli?
Je, jambo hili lina kasoro?
Host 1: Na pia je, swala hili linastahili Heshima?
Je, swala hili linapendeza na je, linafaa kufanywa?
Host 2: Kweli! Na tunapokuwa waangalifu na kile tunachoweka akilini, tunaweza kung’amua mipango ya mungu ni ipi kuhusu jinsi tunafaa kuishi.
Host 1: Naam. Kuna kitu kinaitwa GIGO—garbage in, garbage out. yaani taka ndani, taka nje. Tunapolisha akili zetu na vitu vibaya, inaathiri jinsi tunavyofikiria, tunachonena, tunachotaka na tunachokifanya.
Host 2: pia Stefano nina mtazamo GIGO yaweza kuwa good in, good out. Yaani zuri ndani, zuri nje. (laughing)
Host 1: (Laughing) au God’s ways in, God’s ways out. Njia ya Mungu ndani, njia ya Mungu nje.
Host 2: umeisema vizuri sana. Maana za GIGO zipo nyingi kichwani. Lakini wacha ni kurejeshe nyuma kidogo, hapo awali ulitaja simu za kisasa yaani Smartphones. Nafikiri tunafaa kuzungumza zaidi kuhusu jinsi Mungu anavyotuelekeza kupitia simu hizi.
Host 1: Muhimu sana. Kuna mstari kwenye Bibilia usemao “sitatawaliwa na chochote” (1 Corinthians 6:12) simu yaweza kuwa baraka, lakini kwa wengi sisi vijana, yaweza kutawala maisha yetu iwapo tutairuhusu.
Host 2: Kweli! Wengi wetu tupo kwenye simu zetu kwa masaa matano au zaidi kila siku.
Host 1: lakini simu sio mbaya vile! Kupitia simu zetu, tunauwezo wa kuwasiliana na watu wengine kote duniani. Tunawasiliana kwa kujuliana hali, au pia kueneza jumbe za kutiana moyo.
Host 1: kwa kweli, simu sio mbaya, lakini kuchuku muda mrefu kwenye mitandao ya kijamii, kunaathiri vibaya maisha ya vijana wengi. Kwa mfano, kuna kejeli za mitandaoni- pale baadhi ya watu hunena mabaya kuhusu wenzao. Pia kutuma jumbe na picha za ngono. Picha na jumbe hizi huathiri hadhi yetu na pia huathiri uwezekano wa kupata ajira siku za usoni.
Host 2: Pia afya ya akili inaathirika. Simu za kisasa yaani smartphones, zinewapelekea vijana wengi kuwa na ukosefu wa usingizi, hofu, msongo wa mawazo, upweke, na huzuni.
Host 1: Kweli, na hatufai kuruhusu vifaa kututawala. Ni Sawa na uraibu. Kila tunapopokea jumbe au ishara za kupongeza kazi zetu, akili huachilia kemikali ya dopamine, inayotufanya kuhisi vizuri. Hisia hizi zinatupatia sisi vijana uraibu mkubwa wa simu. Na tunapotegemea sana hisia zitokanazo na dopamine, tunaanza kuwa na upweke na wenye huzuni na tunakosa kufurahia maisha yetu.
Host 2: Tunahitaji usaidizi ili tusiwe wakutawaliwa na simu zetu.
Stefano, ni usaidizi upi unaotufaa sisi vijana kwa ajili ya athari za simu?
Host 1: Kwa jua ni mtandao upi wa kijamii wakujiunga nao, na ni kina nani wa kufuatilia. Usiwahi sema mabaya kumhusu mtu kwenye simu na usisambaze picha za uchi kwa mtu yeyote. Pia ni vyema kumjulisha mzazi kuhusu unachoposti au unachotazama.
Host 2: Kuna mengine rahisi:
Zima simu yako wakati wa mlo na familia.
Usiangalie simu yako kabla ya kulala—itaathiri usingizi wako.
Usilale karibu na simu yako. sleep next to your phone—iweke chaji katika chumba kingine ikiwezekana.
Weka simu yako chini unapozungumza na mwenzio ana kwa ana. Ni heshima kumtazama mtu machoni mnapozungumza.
Host 1: Wenzangu hebu wekeni simu chini kwa dakika moja. Hutaathirika kwa vyovyote. Nimeelimika zaidi kuhusu matumizi bora na salama ya vyombo vya habari haswa simu ya rukono.
Na tunapozungumza kuhusu vyombo vya habari, unaweza kuwasiliana na vijana wengine na kuwapa ujumbe kuhusu matumizi ya vyombo vya habari. Unaweza kudowloadi Application yetu ya Reach for Life au Afikio la Kuishi kupitia App Store au google play store.
Host 2: Pia unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja iwapo una swali, himizo au ujumbe na pia iwapo ungetaka kuwasiliana na washauri wetu wa Afikio la Kuishi yaani Reach for Life. Nambari yetu ni -
Host1 : Pia unaweza kuendeleza mjadala huu kwenye mtandao wetu wa Facebook. Mtandao wetu wa Facebook ukiwa ni R4L Kenya ndio Facebook ni R4L Kenya. Jiunge nasi ili tufunzane kwa pamoja. Pia usisahau tuna zawadi kwa ajili yako. Wasiliana nasi sasa. Duuuh Wambui, tazama muda unavyosonga! Masaa yanakasi sana haswa unapoenjoy somo kama la leo. *Na subiri sana hatua ya pili ya safari ya maisha yaani live journey. Tutaangazia makubwa na madogo.
Host 2: .. Yes, Kweli Stefano tutaangazia we the highs and lows kuhusu uraibu wa pombe na mihadarati. Usikose meenzangu. Tegea papa hapa kwenye stesheni hii wakati na wasaa kama huu wiki ijayo. Jina langu ni Wambui Ngare na nina Afikio la Kuishi.
Host 1: Nami ni Kaindo Stefano nami pia nina Afikio la Kuishi. Endelea Kuafikia Kuishi.
Host 1 and 2: Chaguo ni lako.
Host 2: Hadi wakati mwingine, kwaheri!
Music